Maafisa nchini Marekani wamesema makombora aina ya Tomahawk takriban 60 yame fyatuliwa kutoka meli zakijeshi ambazo ziko katika bahari la Mediterranea.
Hili ni shambulizi la kwanza dhidi ya serikali ya Syria, pamoja na agizo kuu lakijeshi la Donald Trump tokea alipo apishwa kuwa rais.
Makombora dazeni ya Tomahawk, yame gonga ndege za Syria, uwanja wa jeshi la Syria, pamoja na vituo vya mafuta vinavyo dhibitiwa na jeshi la Syria katika uwanja wa ndege wa Al-Sharyat ambao uko karibu ya mji wa Homs magharibi mwa nchi hiyo. Katika kauli fupi, Rais wa Marekani Donald Trump amedai, uwanja huo ulitumiwa kufanya shambulizi la kemikali mapema wiki hii, naku uwa raia wengi katika maeneo ya kaskazini Syria.
Bw Trump ameongezea kuwa, "Rais Wa Syria Bashar al-Assad, ndiye aliye agiza shambulizi hilo".
Kabla ya shambulizi hilo, wawakilishi wa Urusi na Marekani, walikuwa wamekabiliana ndani ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuhusu maneno yatakayo tumiwa katika azimio laku kosoa shambulizi hilo la awali la kemikali.
Chansela wa Ugerumani Angela Merkel amekosoa baraza la usalama kwaku feli kuafikiana.
Share

