Vizuizi vimewekwa kwa mikusanyiko na amri yakuvaa barakoa katika maeneo pana ya Sydney imerejeshwa tena. Mamlaka wa afya wanaendelea kuongeza juhudi zaku dhibiti aina ambukizi sana ya coronavirus kwa jina la Delta, makatazo hayo yakutoka nje pamoja na amri yakuvaa barakoa, inatarajiwa itasalia hadi 2 Julai 2021 kwa maeneo pana ya Sydney pamoja na maeneo kama; Central Coast, Blue Mountains, Wollongong na Shellharbour.
Mtu yeyote anaye ishi au anaye fanya kazi katika vitongoji vya Woollahra, Waverley, Randwick, na City of Sydney, ataruhusiwa tu kutoka nyumbani kwake akiwa na sababu muhimu. Baadhi ya sababu hizo ni: kununua vifaa muhimu, kufanya kazi au kwenda shuleni kama kazi hiyo au hawezi somea nyumbani, kupokea au kutoa huduma, na kufanya mazoezi katika vikundi vya watu 10 au wachache.
Vizuizi hivyo vitasalia hadi usiku wamanane wa 2 Julai 2021.