Vituo vya kupigia kura Australia vimefunguliwa kwa mamilioni ya wapiga kura kuchagua washindi na walioshindwa katika uchaguzi wa shirikisho 2019.
Zaidi ya milioni 16 wanatarajiwa kushiriki katika kura za kitaifa katika maeneo 7,000 ya kupigia kura nchini kote.
'Utakuwa usiku mrefu'

Prime Minister Scott Morrison takes part in an election day sausage sizzle in Launceston, Tasmania. (AAP) Source: AAP
Bwana Morrison anatembelea vituo viwili vya kupigia kura kaskazini mwa Tasmania. Kisha atasafiri nyumbani kwa wapiga kura wa Sutherland Shire mjini Sydney, kabla ya kupiga kampeini na wabunge wengine wa Liberal katika viti vidogo mjini.
"Nadhani itakuwa usiku mrefu. Nimekuwa nikisema kuwa uchaguzi huu utakuwa wa mchuano mkali," Bwana Morrison aliiambia shirika la habari la Seven katika kipindi cha Sunrise leo Jumamosi.
"Wiki tano zilizopita watu hawakusema hivyo lakini siku zote nimetambua kuwa ni mchuano mkali," alisema.
Kiongozi wa Labor Bill Shorten anatarajia kutembelea viti vinavyogombaniwa katika eneo la muhimu la ushindani la Victoria.

Labor Leader Bill Shorten starts election day. Source: Getty
Bwana Shorten alianza siku kwa kukimbia mchakamchaka kuzunguka Melbourne huku akiwa amevaa fulana iliyokuwa na maandishi ya kauli mbiu "Piga kura 1 Mume wa Chloe Shorten".
"Ninachokijua baada ya siku 2000 katika kazi hii ni kwamba, nina ujasiri Labor itaweza kuendesha serikali ya umoja," aliiambia Sunrise.
Kiongozi wa upinzani alipiga kura katika wapiga kura wake wa Maribyrnong magharibi mwa Melbourne.
Kupiga kura-Mapema

Bill Shorten vs Scott Morrison Source: Getty
Hii inalinganisha na jumla ya kura milioni 2.5 katika hatua sawa ya uchaguzi wa shirikisho wa 2016.
Kwa kuongeza, kumekuwa na maombi ya kura milioni 1.5 za posta, Tume ya uchaguzi AEC walisema.