Upigaji kura umemalizika katika uchaguzi wa kitaifa wa Afrika Kusini

Upigaji kura umefungwa katika uchaguzi wa kitaifa wa Afrika Kusini, na matokeo ya awali yanaweza kutokea leo Alhamisi na mshindi rasmi kutangazwa Jumamosi.

Voters will head to the polls in South Africa

South Africa's economic outlook is foggy, if not grim. Source: SBS

Uchaguzi umemalizika Jumatano nchini Afrika Kusini baada ya uchaguzi wa taifa ambao karibia uiweke ANC kuendelea madarakani licha ya hasira juu ya kashfa ya rushwa, ukuaji wa uchumi, na rekodi ya ukosefu wa ajira.

Uchaguzi ni kipimo cha kwanza cha Rais Cyril Ramaphosa kama ataweza kuimarisha msaada kwa chama ambacho msaada wake unatokana kwa kiasi kikubwa na sifa zake za ukombozi, lakini sasa kinakabiliwa na matarajio ya idadi ndogo.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi na wapiga kura milioni 26.8 waliosajiliwa ili kupiga kura zao katika vituo vya kupigia kura 22,925 nchini kote na upigaji kura kufanyika bila ya tukio lolote, viongozi walisema.

Matokeo ya awali yatatolewa leo Alhamisi, na mshindi rasmi atatangazwa siku ya Jumamosi.

Ukosefu wa ajira na madai ya rushwa

Hasira juu ya rushwa, uchumi na mageuzi ya ardhi ni masuala muhimu ikiwa Waafrika Kusini wanapiga kura katika uchaguzi wa sita wa kidemokrasia tangu Ugawanyikaji ulipokoma miaka 25 iliyopita.
South Africa Elections:Unemployment
Waiting for work has become worse in South Africa. Source: SBS
African National Congress, au ANC, ambayo iliongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, iliiongoza nchi tangu mwaka 1994 - lakini inazidi kuwa haipendwi baada ya orodha ya muda mrefu ya viongozi wa ANC walioshutumiwa na rushwa na uharibifu ulioletelea matatizo ya uchumi.

Nchini Afrika Kusini, uchumi unaendelea kuyumba, deni la kitaifa linatia wasiwasi, ukosefu wa ajira ni rasmi liko kwa asilimia 27 na zaidi ya mmoja kati ya vijana wawili hawana kazi.


Share

Published

Updated

By Dubravka Voloder
Presented by Frank Mtao
Source: SBS News, AFP - SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service