Viongozi wa vyama vikubwa walikabiliana katika mijadala ya uchaguzi mkuu, ambako kila mmoja wao alitangazwa mshindi wa mjadala huo, ila hukumu halisi ni ile ambayo inatolewa na wapiga kura katika vituo mbali mbali vyakupigia kura kote nchini.
Waziri Mkuu Scott Morrison, akiwa katika kampeni ya uchaguzi mkuu. Source: AAP
Waziri Mkuu Scott Morrisson amesisitiza kuwa yeye ndiye chaguo bora, lakuendelea kuongoza taifa katika wakati huu ambao Australia inaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Image
Hata hivyo, Kiongozi wa Upinzani Anthony Albanese, amesisitiza kuwa chama cha Labor ndicho chenye sera na nia halisi yakubalisha maisha ya wananchi wote.
Idhaa ya Kiswahili ya SBS itachapisha matokeo ya uchaguzi mkuu punde tutakapo yapata.