Wataalam wana kadiria kuwa itagharimu maeneo husika ya mafuriko hayo ma bilioni yama dola, kukarabati miundombinu mhimu iliyo haribika, bila kutaja mali za watu zilizo potea nakuharibika katika tukio hilo.
Jimboni Queensland Mama Idrissa alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS kwamba, "nguo zote za watoto zime haribika, carpet ndani ya nyumba ime lowa, na itabidi nitupe vitu vingi ambavyo vimeharibiwa na maji pamoja nakusafisha kila sehemu ili kuondoa uchafu na harufu mbaya ambayo ime jaa ndani ya nyumba. Pia itabidi nitupe kila kitu ambacho kiko ndani ya friji kwa sababu vyote viliharibika baada ya umeme kukatwa kwa zaidi ya siku tatu".

Maafisa wa jeshi la Ulinzi wa Australia, wasaidia katika shughuli yausafi baada ya mafuriko kusababisha uharibifu mkubwa mjini Lismore. Source: AAP / Jason O'Brien
Katika mji wa Lismore, barabara nyingi zilijaa taka zilizo tolewa ndani ya nyumba, na majengo ambayo yalikuwa yame zama chini ya maji ya mafuriko. Tatizo kubwa ambalo watu wengi katika maeneo husika ya mafuriko hayo wanakabiliana nalo ni kwamba wengi wao hawakuwa na bima. Licha ya serikali za shirikisho na jimbo kuahidi wahanga msaada wa fela, wengi wanahisi msaada huo ni mdogo sana na wana hofu hawata weza rejesha maisha yao katika hali ilivyo kuwa kabla.
Share

