Watumiaji wa WhatsApp katika nchi kama France, India, Australia na Uingereza ni miongoni mwa wateja ambao wanakabiliana na changamoto zakutumia App hiyo.
"Tunafahamu baadhi ya watu kwa sasa wanakabiliwa kwa wakati mgumu, kutuma nakupokea ujumbe na tunafanya tuwezavyo kurejesha matumizi ya WhatsApp kwa kila mtu haraka iwezekanavyo", kampuni mzazi ya WhatsApp, Meta Platforms imenukuliwa katika maandishi.
WhatsApp ina zaidi ya wateja bilioni mbili, katika zaidi ya nchi mia moja themanini (180) kote duniani.