Nyimbo za Sfiso Ncune zimetumiwa mara nyingi kuwafariji wanao kabiliana na matatizo na wakati mgumu kimaisha. Vizazi vingi pia vime tumia nyimbo zake kama mwongozo wa maisha.
Kuelewa zaidi mchango wa Sfiso Ncune katika sekta ya muziki wa injili, SBS Swahili ilizungumza na Rajabu ambaye ni msanii wa injili anaye ishi Brisbane, na pia alikuwa rafiki wa Sfiso. Bw Rajabu alifafanua pengo ambalo Sfiso Ncune ameacha katika sekta ya muziki wa injili barani Afrika.
