Tamasha ya Africultures ili anza kama wazo la kuleta pamoja jamii zawa Afrika kuchangia tamaduni zao pamoja na marafiki wapya na jamii pana katika nchi yao mpya.
Tamasha hiyo kwa sasa ime kuwa kwa umaarufu, kiasi kwamba kwa sasa ina nafasi yakipekee katika kalenda yamatukio mkoani NSW, Australia, ambako watu husafiri kutoka maeneo ya kanda na mikoa ya karibu kushiriki katika hafla hiyo.
SBS Swahili ilizungumza na baadhi ya waanzilishi na walio hudhuria tamasha yakuadhimisha miaka 10 ya Africultures.
Share






