Walimu wengi ambao si wazawa wa maeneo karibu ya mpaka wa Kenya na Somalia, wame wasilisha maombi yauhamisho baada ya wenzao ku uawa kinyama na wao wenyewe kushambuliwa pia, kiasi kwamba wame kataa kurejea kazini.
George Musamali alikuwa katika kitengo maalum cha polisi ya Kenya zamani. Kwa sasa ni mchambuzi wa maswala ya ulinzi na usalama nchini Kenya pamoja naku ongoza kampuni inayo toa huduma ya ulinzi binafsi.
Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, ali tuarifu kuhusu hali tete ya usalama nchini Kenya ambako mamlaka inakabiliana na vikundi tofauti nchini pamoja na kile cha Al Shabaab.