Angella Okutoyi binti mwenye asili ya Kenya, alibadili hali hiyo katika viwanja vya tennis mjini Melbourne, Victoria ambako, alipeperusha bendera ya Kenya na Afrika Mashariki kwa fahari kubwa, nakuwaacha wapinzani wake pabaya.

Angella Okutoyi katika mechi yake dhidi ya Federica Urgesi wa Italy Source: Getty
Alipozungumza na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Angella alitueleza jinsi mjomba wake alivyo mshawishi nakumfunza kucheza tennis akiwa na umri wa miaka minne, mipango yake yakuwa mchezaji wakulipwa wa tennis, pamoja na maono yake kwa siku za usoni katika tennis.