Maoni ya David Gillespie yamejiri wakati idadi ya wabunge wa serikali ya mseto, wanadokeza mageuzi yafanywe kwa viza za kazi ili ziwazuie wahamiaji na wakimbizi waliofadhiliwa na waajiri katika maeneo ya kanda, kutoondoka katika maeneo hayo nakuhamia katika maeneo ya miji baadae.
Miji kadhaa kandani imefanikiwa kuendeleza kazi katika viwanda na sekta kadhaa, kupitia wafanyakazi kutoka mazingira ya ukimbizi.
Kwa mfano, zaidi ya idadi ya wakimbizi mia moja kutoka Myanmar wanafanya kazi katika mji wa Nhill mkoani Victoria, wengi wao wanafanya kazi katika viwanda vya uzalishaji wa kuku.