Baada ya miongo ya ukame na ukosefu wa timu kutoka bara la Afrika kuto shiriki katika nusu fainali ya kombe la dunia, hatimae Morocco imemalizia bara la Afrika kiu hicho baada yakushinda mechi yao ya robo fainali dhidi ya timu ya Ureno katika robo fainali.
Ushindi huo ume ipa Morocco fursa kuwania nafasi katika fainali ya kombe la dunia, ila itabidi wakabiliane na mtihani mkali kutoka bingwa watetezi Ufaransa katika nusu fainali ya kombe hilo.
Bw Athiei na Akram, nima nahodha wa timu za Sudan Kusini na Jamhuri ya Congo, timu zao hucheza katika kombe la Afrika mjini Sydney.
Wawili hao walieleza SBS Swahili hisia zao wakati wa mechi ya robo fainali kati ya Ureno na Morocco pamoja na matarajio yao kwa mechi ya nusu fainali dhidi ya Ufaransa. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.