Australia imejibu shambulizi hilo kwaku wafukuza wanadiplomasia wawili wa Urusi. Serikali imesema ina amini wawili hao ni majasusi ambao hawaja sajiliwa. Hatua hiyo ni simbamba na hatua zilizo chukuliwa na mataifa ya magharibi kama jibu kwa shambulizi hilo.
Hata hivyo, mamlaka ya Urusi ime endelea kusisitiza kuwa haina hatia kuhusiana na swala shambulizi hilo.
Menna Rawlings ndiye balozi wa uingereza nchini Australia, amekaribisha tangazo hilo.
Peter Jennings ni mchambuzi wa maswala ya usalama wa taifa kutoka shirika la Australian Strategic Policy Institute, Bw Jennings amesema hakuna shaka Urusi itajibu hatua hizo, kwaku wafukuza baadhi yama balozi wa Australia.