Waziri Mkuu Anthony Albanese amependekeza mageuzi kwa katiba, wakati Australia inachukua hatua zakihistoria zakuwa na sauti ya watu wa asili bungeni.
Waziri Mkuu Anthony Albanese ameweka wazi maneno yatakayo tumiwa katika swali ambalo wa Australia wata ulizwa, katika kura ya maoni kwa kutambuliwa kwa watu wa asili wa katika katiba.
Watu wataulizwa, "Una unga mkono mageuzi kwa katiba yanayo toa sauti kwa wa Aboriginal nawatu wa Torres Strait Islanders?"
Kura ya maoni ikiendelea mbele, itakuwa ya kwanza katika zaidi ya miaka 20. Ni kura za maoni 8 tu kati ya 44 ambazo zimefanikiwa nchini Australia tangu mwaka wa 1901.
Share






