Biashara za Australia, vyuo pamoja na wanao toa huduma ya afya, wanatarajiwa kufaidi kupitia mkataba huo, wakati huo huo serikali ya shirikisho inajaribu kuboresha mahusiano yake na China.
Kando na biashara ya bidhaa, maafikiano hayo yanatoa sheria sawia kwa biashara yakidijitali, pamoja na haki miliki.Mkataba huo pia utatoa upatikanaji bora kwa sekta za huduma za Australia kama, huduma zakifedha, huduma ya afya pamoja na elimu.
Makundi yakibiashara nayo yamesema kuwa mkataba huo wakibiashara ni muhimu, kwa uponaji wa Australia kutoka kutikisishwa kwa uchumi ambako kulisababishwa na janga la COVID-19.