Jumatatu polisi wa Uganda walifyatua risasi nakutumia gesi zakutoa machozi, kuwatawanya waandamanaji ambao wanataka msanii maarufu ambaye ni mwanasiasa pia Bobi Wine, ambaye amekuwa mkosoaji mkuu wa Rais Yoweri Museveni aachiwe huru, pamoja na wabunge wenzake na wanaharakati walio kamatwa pia.
Polisi wa Uganda wame thibitisha kuwa wamekamata watu wapatao 103, ambao walihusika katika maandamano baada ya mbunge Robert Kyagulanyi na wabunge wenzake pamoja na wanaharakati kuwekwa vizuizini. Imeripotiwa pia, kuwa mtu mmoja ame uawa katika maandamano hayo.
SBS Swahili ilizungumza na mgombea wa zamani wa udiwani katika halmashauri ya jiji la Logan, Queensland, Blaise Itabelo kuhusu hali ilivyo mjini Kampala, Uganda.