Biashara kubwa pia zita unda mfuko wa akiba, kwa niaba ya watoto wa wazima moto walio fariki kazini.
Tamasha ya afueni ya moto wa vichaka itafanywa mwezi ujao katika eneo la michezo na burudani la Sydney Olympic Park. Wasanii maarufu watakao tumbuiza katika tamasha hiyo bado hawaja tangazwa, ila kuna uvumi kuwa msanii Queen ambaye sehemu ya wimbo wake umeusikio muda mfupi ulio pita atashiriki. Bendi hiyo itakuwa nchini Australia, ikifanya tamasha ndani ya ukumbi huo siku moja kabla ya tamasha hiyo.
Licha ya orodha ya wasanii watakao shiriki kutojulikana, kilicho wazi ni kwamba michango itahitajika, wakati zaidi ya nyumba 2000 kufikia sasa zime haribika.