Swala la ugatuzi nchini Kenya lime zua mvutano mkubwa, katika viwango vyote vyaki siasa nchini humo.
Kaunti ya Nairobi nayo haija achwa nyuma katika mivutano yakisiasa, kiasi kwamba spika wa bunge ya kaunti hiyo amekuwa jeruhi mpya wamivutano hiyo. Baada yakukabiliwa kwa upinzani dhidi ya uongozi wake kwa muda mrefu, hatimae ali amua kujiuzulu na wadhifa wake kuchukuliwa na diwani mwingine kwa haraka.
Bw Ben Mulwa ndiye msemaji wa gavana wa kaunti ya Nairobi, katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, alifunguka kuhusu miradi ambayo gavana wa Nairobi anaongoza kuboresha maisha ya wakazi wa kaunti hiyo, pamoja na misukosuko yakisiasa ambayo ime ibuka kupitia swala la ugatuzi nchini humo.
Share





