Vilabu vinavyo shiriki katika ligi kuu ya soka ya Uingereza haswa Manchester United, vina ma milioni ya mashabiki kote duniani.
Bill ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa Manchester United (Man Utd), ambaye katika miaka ya hivi karibuni amekuwa aki kabiliwa kwa wakati mgumu timu yake inapo ingia dimbani ambako mara nyingi imekuwa ikishushiwa vichapo. Licha ya dozi za huzuni ambazo timu yake imekuwa ikimpa, Bw Bill alieleza SBS Swahili kwamba
"Man Utd ni sehemu ya utambulisho wangu, na siwezi shabikia timu nyingine."
Licha ya hiyo Bw Bill hakusita kufika katika dimba la Melbourne Cricket Ground (MCG) ambako alijumuika pamoja na maelfu yamashabiki wenza kushuhudia timu yake pendwa iki menyana na Crystal Palace kabla ya ligi kuu ya Uingereza kuanza tena. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Bw Bill alifunguka kuhusu mapenzi yake na timu hiyo pamoja nakutabiri matokeo ya mechi ambayo alikuwa anaenda kushuhudia.