Wana jumuiya yawa Tanzania wanao ishi mjini Melbourne, Victoria wanajiandaa kushiriki katika sherehe kubwa ya uhuru wa taifa lao pendwa.
Bw Ary Lyimo ni mmoja wa waanzilishi wa jumuiya hiyo, na kwa sasa ni mshauri wa baraza la uongozi wa jumuiya hiyo.
Katika mahojiano na SBS Swahili, Bw Ary alifunguka kuhusu mchango wa jumuiya yake katika jumuiya pana ya Australia, pamoja na vitu wanajumuiya na marafiki wao wanastahili tarajia siku ya sherehe.

Unaweza pata taarifa zaidi kuhusu sherehe hiyo, pamoja na matukio mengine ya jumuiya yawa Tanzania kwenye kurasa zao za mitandao yakijamii: Tanzanian Community Association of Victoria INC. Australia.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.






