Nchini Australia sawia na katika sehemu zingine za dunia sherehe zakufunga mwaka, au kusherehekea mafanikio watu na mashirika mbali mbali yali pata katika mwaka huo ni kawaida.
Bw Kisimba ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la Joining Families Support Services. Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, alifunguka kuhusu sababu zaku andaa sherehe ya krismasi yawa Afrika jimboni New South Wales.
Bw Kisimaba aliweka wazi pia baadhi ya mafanikio ambayo sherika lake la JFSS ambalo lilidhamini sherehe hiyo, lilipata katika mwaka huu wa 2022.
Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma za shirika la Joining Families Support Services bonyeza hapa: https://www.joiningfamilies.org/