Afueni imerejea katika mitaa ya mji wa Bouake, ambao ndio mji mkuu wa pili wa Ivory Coast baada ya wanajeshi kufanya uasi kwa siku mbili, mgomo ambao ulisambaa nchini kote.
Alassane Outtara ndiye rais wa Ivory Coast, ameafiki baadhi ya madai ya wanajeshi hao kuhusu malipo na mazingira ya kazi.
Hata hivyo, kisa hicho kimezua wasi wasi miongoni mwa wenyeji, na wanamhamasisha rais wao ahakikishe kisa hicho kisirudiwe tena.
Share
