Seneta mmoja ambaye alikuwa hajulikani sana, kabla atoe hotuba yake ya kwanza ndani ya seneti, alijipa umaarufu nchini kote kwaku pendekeza marufuku ya wahamiaji ambao ni waislamu.
Wakati huo huo sera muhimu ya serikali kwa nishati, ilipita kizuizi cha kwanza kwaku kubaliwa katika mkutano wa chama tawala.
Hotuba ya seneta huyo pamoja na sera ya nishati ya serikali, zili zua utata hata kama swala moja lilifunika lingine kwa ukali wa ukosoaji.
Wakati wanachama wa serikali ya mseto, wanaweza piga kura kwa hiari yao, itaonekana vibaya kwa serikali iwapo baadhi yao wata vuka sakafu kupiga kura dhidi ya sera ya dhamana ya nishati.
Muswada huo unatarajiwa kufikishwa bungeni, katika vikao vya kwanza viwili, utakapo idhinishwa na serikali za mikoa na majimbo.