Serikali ya Morrison pia ilipigia debe ziada ya bajeti ambayo chama cha Labor imesema, inakuja kwa gharama ya uwekezaji kwa mfumo wa dhamana ya ulemavu wakitaifa.
Wiki hii pia waziri wa maswala ya nyumbani Peter Dutton aliwasilisha sheria bungeni, yenye lengo lakufanya iwerahisi kufuta uraia wa mtu ambaye ana uraia wa nchi mbili, ambaye amepatwa na hatia ya makosa ya ugaidi.
Ila mtumishi wa umma mwenye wajibu wakufuatilia sheria za ulinzi wa Australia James Renwick alisema kwamba, sheria hiyo haija dhibitiwa kwa hali yake ya sasa na ameomba ifutwe.
Wakati huo huo waziri mkuu Scott Morrison amemaliza wiki hii akiwa nchini Marekani, ambako anakutana na rais wa Marekani Donald Trump, pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu katika ikulu ya Marekani.
Bunge litakuwa katika mapumziko kati ya Septemba 20 hadi Oktoba 7 2019.