Ilikuwa pia fursa kwa sura mpya, kujitambulisha kupitia hotuba zao za kwanza.
Katika taarifa zingine Bw Morrison ametangaza kuwa, kiongozi wake wa zamani wa wafanyakazi na hazina Phil Gaetjens, ata ongoza idara ya waziri mkuu na baraza la mawaziri baada yakuthibitisha kuwa Martin Parkinson ata jiuzulu.
Mwisho lakini muhimu, licha ya upinzani wa serikali, seneti ilipigia kura uchunguzi uanzishwe kuchunguza utoshelevu wa malipo ya Newstart, wakati kuna ongezeko la wito kwa kiwango cha malipo hayo kiongezwe, kwa sababu hakija panda juu ya mfumuko wa bei tangu mwaka wa 1994.