Bw Mmombwa alisaidia timu yake ya Macarthur FC kufuzu kwa fainali ya kombe la Australia na siku chache zilizopita alijiunga na wachezaji wenzake pamoja na mashabiki wao katika sherehe baada yakushinda kombe hilo.

Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Bw Mmombwa alifunguka kuhusu juhudi anayo weka kuhakikisha anasalia katika kiwango bora ili achaguliwe na mwalimu kucheza, pamoja na anavyo kabiliana na shinikizo la kuwa balozi wa jamii yawa Afrika uwanjani.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.