Vijana kutoka jamii ya D R Congo wanaingia dimbani leo dhidi ya Misri, katika mechi yao ya kwanza ya kombe la Afrika jijini Sydney, Australia.
D R Congo ni mshindi wa zamani wa kombe hilo sawa na Misri, hata hivyo nahodha wa D R Congo Clement alieleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS kwamba, vijana wake wame jiandaa ipaswavyo na wako tayari kupata ushindi katika mechi yao ya kwanza ya kombe hilo.
Mechi ya D R Congo dhidi ya Misri ita anza saa kumi na moja jioni masaa ya mashariki ya Australia, katika uwanja wa Western Sydney Football Centre, Eastern Road, Rooty Hill, New South Wales, Australia.
Share






