Vijana wa D R Congo wali ingia dimbani dhidi ya Misri katika mechi ambayo, kihistoria huwa na changamoto zake na licha ya DR Congo kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa na ushindi wa goli moja kwa sufuri, vijana wa Misri walionesha umahiri wao kwa kuzuia miamba ya DR Congo kuwatatiza.
Kipindi cha pili cha mechi hiyo kilianza sawia na kile cha kwanza, hali ambayo ilianza kuzua tumbo joto miongoni mwa mashabiki wa timu hizo mbili. Licha ya pandashuka za mechi hiyo, vijana wa DR Congo walionesha umahiri wao nakushinda mechi hiyo kwa magoli 4 kwa 1 ya Misri.
Punde baada ya mechi hiyo kuisha, mashabiki pamoja na nahodha wa DR Congo wali eleza Idhaa ya Kiswahili ya SBS hisia zao kwa mechi hiyo. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.