Wanaharakati wanao tetea haki za walemavu wamesema, wa Australia wanastahili tarajia kusikia hadithi zakutisha, katika vikao vya tume hiyo.
Ila idadi inayo endelea kuongezeka ya wanaharakati wengine, wanasema wanaweza kosa kuhudhuria vikao hivyo ambavyo vimesubiriwa kwa muda wa miaka mitatu, kwa sababu ya shutma za mgongano wa maslahi.
Makamishna wa tume hiyo, wame elezwa watoe ripoti ya kwanza kufikia tarehe 30 Oktoba mwaka wa 2020, na ripoti ya mwisho itatolewa tarehe 29 Aprili mwaka wa 2022.
Uchunguzi huo utafanyiwa Brisbane ila, vikao vyake vita pelekwa nchini kote. Watu wanaweza pia toa ushahidi wao mtandaoni.
Na kama wewe au mtu unaye jua anahitaji msaada, unaweza pigia simu mashirika kama Lifeline kwa namba hii 13 11 14 na Dhulma ya ulemavu ya kitaifa nakupuuza kwa namba hii 1800 880 052.