Hiyo inafuata, baada ya Marekani kuamua kuizuia Huawei kwenye soko la Marekani na kupiga marufuku mauzo ya teknolojia ya Marekani na vifaa kwa kampuni hiyo, China iliionya Washington dhidi ya vikwazo zaidi vya mahusiano ya kibiashara.
Frank Mtao alikutana na wataalam watatu ambao wanafanya kazi katika nyanja tofauti kuhusiana na biashara na mawasiliano ili kujadili juu ya mvutano huu kutoka kwa mataifa makubwa.