Wakati hufika ambapo mtu lazima ajifunze lugha mpya kwa ajili yakushiriki katika mazungumzo kwa ufanisi, pamoja nakuchangia ujumbe anao taka toa.
Kama sehemu ya mashindano yakitaifa ya lugha ya SBS, idhaa yakiswahili ya SBS ilitembelea shule yakijamii yakiswahili mjini Newcastle NSW, ambako wanafunzi ambao wana asili ya Afrika mashariki wame pewa fursa yakujifunza moja ya lugha ya taifa ya zaidi ya nchi 4 barani Afrika.
Wazazi, wanafunzi na mwalimu wa shule hiyo, wali eleza Idhaa ya Kiswahili kuhusu uzoefu wao wakijifunza Kiswahili katika shule hiyo.