Ila, si wote ambao ndoto zao hutimia. Dor Jok ni mmoja wa vijana wenye asili ya Sudan Kusini kutoka Perth, Magharibi Australia.
Jamii ya watu kutoka Sudan Kusini imekuwa ikizalisha vijana wengi wenye vipaji vikubwa ambao wengi wao kwa sasa wanacheza mpira wa miguu wakulipwa Dor Jok akiwa mmoja wao.
Katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, Bw Dor alifunguka kuhusu alivyo pata fursa yakuwa mchezaji wakulipwa pamoja nakutoa hamasa kwa vijana wenza wanao tafuta fursa hizo.
Bw Dor alifunguka pia kuhusu furaha yake, kwa uhamisho wa rafiki yake Garang Kuol kutoka Central Coast Mariners FC, kwenda Newcastle United FC ya Uingereza.