Baadhi ya mifumo hiyo nikupitia kusambazwa kwa taarifa za uongo kuhusu wagombea au vyama pinzani kwa ajili yaku yumbisha imani na uvutio wa wapiga kura wa wagombea/vyama hivyo.
Katika uchaguzi mkuu uliopita nchini Marekani, mashirika, na nchi kadhaa zilishtumiwa kwakushiriki kusambaza taarifa za uongo katika kampeni za uchaguzi wa rais. Douglas ni mtaalam wa maswala ya teknolojia na usalama wa mitandaoni anaye ishi katika jimbo la Arizona nchini Marekani. Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Douglas aliweka wazi jinsi usalama wa mitandao ume imarishwa nchini Marekani haswa wakati huu wa uchaguzi mkuu.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.