Kongamano mjini Sydney lime leta pamoja makundi tofauti, kujadili jinsi yaku kabiliana na tatizo hilo.
Chama cha upinzani cha shirikisho kimeahidi kubadili sheria iwapo kitashinda uchaguzi, na Linda Burney ambaye ni msemaji wa upinzani kwa swala lakuzuia vurugu ya familia, ali eleza kongamano hilo kuwa chama cha Labor kina kubali mapendekezo ya msingi katika ripoti hiyo ya seneti.
Julian Hill ni mbunge wa chama cha Labor, ameiomba serikali ioneshe ujasiri na utu na ichukulie swala hilo hatua. Amesema kwamba msimamo mmoja wakitaifa, unahitajika kutatua tatizo hilo.