Dr Eugen Bacon ni mkaaji wa Melbourne mwenye asili ya Tanzania. Amechapisha kitabu chake cha nane kwa jina la Danged Black Thing, kitabu hicho kina jumuisha hadithi kadhaa kuhusu upendo, uhamiaji, jinsia katika bara la Afrika na ughaibuni.
Katika mazungumzo maalum na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Dr Eugen alitueleza kilicho mshawishi kuwa mwandishi wa vitabu pamoja nakuchangia siri zakufanikiwa kama unataka kuwa mwandishi wa vitabu.
Unaweza wasiliana nakupata maelezo zaidi kuhusu vitabu vya Dr Eugen hapa: www.eugenbacon.com @EugenBacon