Askofu Dkt Fidele Masengo, ni mwanasheria pamoja nakuwa Askofu anaye ongoza kanisa kubwa nchini Rwanda.
Alipomaliza ziara yake nchini Australia siku chache zilizo pita, alizungumza na SBS Swahili ambapo aliweka wazi jinsi taaluma yake ya uanasheria inavyo endana sawa na taaluma yake ya Uaskofu.
Katika mahojiano hayo Askofu Dkt Masengo, alichangia mbinu nne ambazo watu wanaweza tumia kukabiliana na changamoto wanazo pitia katika kila hali ya maisha yao.
Askofu Dkt Masengo ni mwandishi wakitabu kwa jina la: The Marriage of your Dreams (Ndoto ya ndoa yako) ambacho unaweza kipata kwenye tovuti ya Amazon.
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.