Utafiti mpya umebaini kuwa moja kati ya vifo vinne vya kuzama majini nchini Australia, vinawahusu watu ambao walizaliwa ng'ambo.
Ripoti hiyo imejiri wakati zaidi ya shule mia nne za kuwafunza watu kuogelea nchini kote, zinajianda kutoa mafunzo ya kuogelea bila malipo kwa watoto kwa muda wa wiki nzima.
Lengo la kampeni hiyo ni kuongezea uelewa kuhusu usalama majini, kwa watoto wa wahamiaji pamoja na watoto wengine.
Share






