Scott Morrison alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Australia wa thelathini Agosti mwaka jana, baada ya kura ya uongozi ndani ya chama cha Liberal, ikiwa ni baada ya machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya uongozi ndani chama hicho.
Bw Morrison alipewa ajira hiyo baada ya mrengo wakihafidhina wa chama hicho, kushindwa kuvumilia uwezo wa waziri mkuu wa zamani Malcolm Turnbull, kupitisha bungeni sera zake muhimu za nishati namakato ya kodi.
Tangu tukio hilo, imeonekana kama Bw Morrision ameunganisha tena chama cha Liberals, ila kuna baadhi ya wanachama ambao hawana uhakika kama atafanikiwa kuongoza chama cha mseto kupata ushindi katika uchaguzi mkuu.
Share






