Wakati uvumi unaendelea kuzunguka uongozi wake, ambao umesababishwa na sera yake muhimu ya nishati, waziri mkuu Malcolm Turnbull ametangaza mageuzi kadhaa katika pendekezo la dhamana ya nishati ya taifa.
Wanaopinga uwepo wa mabadiliko ya tabia nchi bungeni, wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani Tony Abbott, ambaye alikuwa ame tishia kuvuka sakafu kupiga kura dhidi ya sera hiyo, kama ingejumuisha kumbukumbu yoyote ya malengo ya uzalishaji wa 26% ya hewa chafu, kama ilivyo kubaliwa katika mkataba wa mazingira wa paris.
Wabunge wa vyama vya mseto vya Nationals na Liberals wame karibisha sera hiyo mpya, ila upinzani umesema mageuzi hayo yame fanywa kuwatuliza wapinzani wenye misimamo mikali, ndani ya chama tawala cha mseto.
Share






