Baadhi yao wamefanya hivyo kwa sababu ya mazingira yasiyo ridhisha katika makampuni ambako wame ajiriwa, wakati wengi wame vutiwa na uhuru wakujiajiri nakutumikia ndoto zao.
Bw Eshima ni mmoja wa vijana hao, ambao wame fanya maamuzi yakujiondoa katika soko la waajiriwa na badala yake, amefungua biashara ambayo imekuwa ikimsaidia kumudu mahitaji yake naya familia yake. Bw Eshima alifunguka katika mazungumzo maalum na SBS Swahili, kuhusu uamuzi wakufungua biashara yake, changamoto ambazo amepata na mafanikio katika biashara hiyo.
Unaweza tazama baadhi ya kazi zake kwenye YouTube yake: Eshima Video TV. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.