Baraza la shirikisho la jamii zenye tamaduni tofauti, limesema kutengwa kwao katika zoezi hilo, kuna zua wasi wasi kuhusu mtazamo wa serikali kwa jamii zenye tamaduni tofauti.
Shirika hilo pia lime toa wito kwa uwekezaji wa ziada wa dola milioni 60, kwa shirika la Tourism Australia, ili liweze shindana vizuri zaidi na nchi zingine.
Mashirika yakimataifa nayo pia yame wasilisha maombi yao kabla ya bajeti kutangazwa, mashirika hayo yame omba viwango vya uwekezaji wa misaada yakigeni ipigwe jeki.
Shirika la Plan International limependekeza kuwa kiwango cha uwekezaji huo, urejeshwe kwa kiwango cha 0.7% ya pato la taifa, pamoja nakuwekeza katika mfumo mpya kwa miondombinu katika ukanda wa pasifiki, ambayo ni kando na bajeti ya msaada wakigeni.
Kile ambacho serikali imewekeza au haijawekeza, kitawekwa wazi kwa umma, saa moja unusu usiku wa Jumanne tarehe 2 Aprili, kwa masaa ya mashariki ya Australia.