Wakati kundi moja la wabunge namaseneta wa chama cha Liberal, walikuwa wakiongoza kampeni yakubadili kiongozi wa chama, ambaye pia ndiye waziri mkuu wa taifa, wabunge wengine namaseneta, walijipata wamezolewa na wimbi la vurugu iliyo ibuka.
Lucy Gichuhi ni Seneta wa jimbo la Kusini Australia wa chama cha Liberal, alishuhudia kwa hali yakipekee jinsi mirengo yakulia nakushoto, ya chama tawala ilivyokuwa ikijiangamiza.