Hali hiyo imeibua wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya afya ya kiakili, na shida zinazo sababishwa na mchezo wa kamari huku wataalam wakiomba msaada zaidi ili waweze saidia watu walio hatarini.
Maoni hayo yametolewa wakati wataalam wa kupunguza madhara, wakishinikiza kuwepo kwa tume ya kifalme katika tasnia ya kamari.
Iwapo wewe au mtu anaye mjuwa anakabiliana na changamoto zinazo sababishwa na kamari, usiwe na hofu, kuna watu na mashirika mengi ambayo yako tayari kutoa msaada wa kila aina kukabiliana na changamoto hizo. Kwa hiyo usijihisi uko mwenyewe, pigia simu nambari hizi kwa msaada utakapo kuwa tayari, 1800 856 800 au wasiliana na shirika la lifeline kupitia namba hii 13 11 14 ambako utapata msaada unao hitaji.