Serikali ya shirikisho ime tangaza mpango ambao unatarajiwa, kuwafikia wa Australia wapatao milioni, wenye miaka kati ya 14 na 19 katika miaka minne ijayo.
Serikali ya shirikisho iko chini ya shinikizo kuorodhesha chanjo ya aina B ya ugonjwa huo, ila chanjo hiyo haiwezi orodheshwa hadi itakapo pendekezwa na kamati ya wataalam. Kampuni ambayo inatengeza chanjo hiyo, ime hamasishwa iombe mradi wa chanjo wa taifa iorodheshe chanjo hiyo.
Mwezi jana wa Agosti kampuni hiyo ilisema ita zingatia, kuchukua hatua hiyo itakapo ona matokeo ya chanjo hiyo Kusini Australia mwaka ujao.