Siku chache zilizo pita, alishiriki katika kampeni yaku elimisha umma kuhusu ugonjwa wa Usonji (Autism).
Kwa mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO):
Ugonjwa wa Usonji kwa kiingereza Autism, ni ugonjwa ambao hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani. Usonji ni tatizo la kibaiolojia analopata mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake, na dalili huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Kabla ya hapo wataalamu wanasema ni aghalabu kuona dalili hizo ambapo zinapojitokeza mtoto hukosa mbinu za uhusiano, anashindwa kuzungumza na wakati mwingine kurukaruka na hata kujing’ata."
Bw George ni mzazi wa mtoto mwenye Usonji, na hiyo ilikuwa moja ya sababu kubwa iliyo mshawishi kushiriki katika kampeni hiyo, kando na uchochezi kutoka kwa baadhi ya marafiki wake.

