Hakuna shaka uamuzi wa Mahakama ya Upeo, kutupa nje maombi ya mrengo wa Azimio One Kenya, kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais nakuidhinisha ushindi wa Dr Ruto ume sababisha mgawanyiko katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Wakenya wanao ishi Australia, wamekuwa wakifuatilia kwa karibu matukio yanayo endelea nchini kwao wengi wao wakichangia hisia zao mtandaoni.
Bw George ni shabiki wa sera za rais mteule Dr William Ruto, licha yakuwa katika hali ya furaha na sherehe, amekiri Dr Ruto anakibarua kigumu kuunganisha taifa ambalo kwa mara nyingine limewaganyika kwa sababu ya matokeo ya urais. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.