Bw Kamerhe amezuiwa kwa tuhuma za ufisadi wa fedha zilizo tengwa kwa ajili yakutekeleza mpango wa siku 100 za rais Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe anashukiwa kwa kosa la ubadhirifu wa fedha za serikali, ila wafuasi wa UNC wanamatumaini na sheria ya Kongo, licha ya kuwa wamekerwa kuona kiongozi kama huyo ametupwa jela badala ya kuwekwa chini ya ulinzi katika kizuizi cha nyumbani.
Licha yakusalia gerezani kwa siku kadhaa, Bw Kamerhe amekana shutma zote dhidi yake. Germain Byadu ndiye kiongozi wa chama cha UNC nchini Australia. Katika mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya SBS, Bw Byadu aliweka wazi masaibu yanayo mkumba kiongozi wa chama chake.