Katika enzi za Sir Alex Furgusson, Manchester United ilikuwa mfalme wa ligi kuu ya Uingereza. Hata kama ilikuw ainapoteza mechi, mashabiki walikuwa na imani kuwa itasawazisha nakupata ushindi katika dakika za lala salama.
Ila siku hizi woga ambao timu zilizokuwa ziki cheza dhidi ya United kabla, ume yayaku na badala ya United kutoa adhabu kwa timu zingine, wao ndiwo wanalisha adhabu na vichapo mara kwa mara siku hizi. Taarifa zime zidi kuvuja kuhusu ukosefu wa imani miongoni mwa wachezaji kwa wenzao, hali ambayo ilikuwa tofauti kabisa katika miaka ya nyuma.
Mchambuzi wetu wa micheoz Herbert Gatamah, alizungumzia swala hili pamoja na mbio zakufuzu kucheza katika mechi za klabu bingwa ulaya, pamoja nakumulika hali ilivyo katika mkia wa ligi ambako kwa sasa timu 5 zinawafanya ziwezavyo kuepuka kushuka daraja mwisho wa msimu huu.