Mfuko huo wenye thamani ya dola bilioni 144 ya makato ya kodi kwa ma milioni yawa Australia, umejiri baada ya ushauriano wa dakika za mwisho na maseneta wa vyama vidogo.
Wakati huo huo chama cha Labor, kime ahidi kuwa iwapo kita shinda uchaguzi mkuu naku unda serikali, chama hicho kita ongeza mara mbili makato ya kodi kwa wenye mapato ya chini pamoja naku itekeleza haraka zaidi kuliko serikali ya mseto.
Chama hicho kime ongezea kuwa kita futa hatua ya pili na tatu ya mpango wa kodi wa serikali. Afueni ya kodi kwa Australia ya kati kwa sasa inaelekea kuwa swala muhimu katika chaguzi dogo tano zijazo mwezi julai pamoja na uchaguzi mkuu wa shirikisho.